Subscribe: KLH News
http://mwanakijiji.podomatic.com/rss2.xml
Added By: Feedage Forager Feedage Grade B rated
Language: Swahili
Tags:
ccj  ccm  cha  chama cha  chama  hata  juu  katika  kuhusu  kuwa  kwa  marmo  mkuu  nchini  sheria  uchaguzi  uongozi  yake 
Rate this Feed
Rate this feedRate this feedRate this feedRate this feedRate this feed
Rate this feed 1 starRate this feed 2 starRate this feed 3 starRate this feed 4 starRate this feed 5 star

Comments (0)

Feed Details and Statistics Feed Statistics
Preview: KLH News

KLH NewsThe most prominent, provocative, and premier Swahili podcast by an author and political analyst M. M. Mwanakijiji and the crew. The podcast is intended to be an instrument that facilitate positive attitudinal and mentality change among Tanzanians as theyPublished: Wed, 13 Dec 2017 19:28:42 +0000

 MAHOJIANO YA DR. SLAA NA ITV YALIYOBADILISHA MWELEKEO!

Fri, 29 Oct 2010 05:33:40 +0000

(image)
Dr. Slaa alipata nafasi ya kuzungumza siku ya Jumamosi na kituo cha Televisheni cha ITV kuhusu masuala mbalimbali ya kampeni na mwelekeo wake wa uchaguzi. Matangazo hayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mawazo ya watu mbalimbali kuhusu Dr. Slaa na kumpatia mashabiki wengine wengi. Hata hivyo marudio ya kipindi hicho tumedokezwa yamepigwa marufuku... Hii ni nafasi ya kuyasikiliza kwa wale ambao hawakupata nafasi.


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-10-28T22_33_40-07_00.mp3
Exclusive: Mahojianona Fred Mpendazoe - Mbunge aliyeikacha CCM na kujiunga CCJ!

Mon, 12 Apr 2010 03:50:38 +0000

(image)
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi! - Nyerere Watanzania bado wana maswali juu ya Chama Cha Jamii (CCJ) hasa kama kweli hiki chama kimekuja kuziba pengo la uongozi nchini au ni geresha tu kama ya vyama vingine. Kabla hata ya kwenda kuomba usajili wa muda tetesi zilishasambaa juu ya ujio wa chama hicho na ndani ya wiki chache tu CCJ kimepata kutangazwa sehemu mbalimbali kwa bure kabisa huku kikivuta mioyo ya wananchi wa kawaida kabisa waliochosha na vyama vya kisiasa vilivyopo ambao kwa muda mrefu wamesubiria kuona matamanio ya Baba wa Taifa kuhusu chama mbadala cha upinzani yakitimia. Tetesi kubwa ni uwepo wa vigogo nyuma ya CCJ na wapo ambao hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe au kufikiri wenyewe kuhusu CCJ hadi waone kwanza nani ameondoka CCM. Kwa wale ambao wanasubiri wasikie “majina makubwa” yakitoka CCM ndio waamini basi kutoka kwa Bw. Fred Mpendazoe hakuwatoshi. Ni wazi vile vile hata likitoka kundi jingine ndani ya CCM bado wapo watu ambao hawataamini na wataendelea kutafutua ufafanuzi kwanini hao siyo “vigogo” au kwanini kuondoka kwao “ni nafuu kwa CCM”. Vyovyote vile ilivyo, Watanzania wana haki na sababu ya kuipima CCJ kwa katiba yake, malengo yake, mapendekezo yake ya kushughulikia masuala ya taifa na itikadi yake. Itakuwa ni upungufu wa hekima, na uwezo wa kufikiri kama tutajaribu kukipima CCJ kwa kuangalia nani “anatoka CCM”! Mtu mwenye hekima atachukua muda kusikiliza kile ambacho uongozi wa CCJ, mashabiki wake, Katiba na watunga sera wake wanasema juu yake na siyo kile ambacho waathirika wa uwepo wa CCJ wanasema juu yake. Hivyo, mahojiano haya ya kwanza na Mhe. Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa CCM wa kuchaguliwa kwa asilimia 81 (kura 64,000) na ambaye ameamua kuondoka CCM “mapema” yatatupa mwanga wa ni watu gani wako nyuma ya CCJ na kama tunaweza kukubali na kukumbatia uwepo wake katika kuendeleza demokrasia nchini na hasa katika kupatia uongozi “bora” ambao taifa limekuwa likiutamani na kuungojea kwa muda mrefu hasa baada ya kukatishwa tamaa na uongozi ulioingia 2005. Sikiliza na uamue mwenyewe.


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-04-11T20_50_38-07_00.mp3
Mchango wa mjadala wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi; Ni sheria mbaya!

Fri, 05 Mar 2010 06:10:40 +0000

(image)
Mapema leo nimeshiriki kwenye mjadala wa Star TV kuhusu sheria iliyopitishwa hivi karibuni ambayo inalengo la kusimamia matumizi ya fedha katika Uchaguzi. Rais Kikwete alitumia hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari kuelezea juu ya uzuri wa sheria hii na kwanini ataitia sahihi kwa mbwembwe kuonesha kuwa anatimiza ahadi yake ya 2005. Kwa maoni yangu sheria hii ni miongoni mwa sheria mbaya na ambayo itatuletea matatizo kuliko Sheria ya Madini ya 1998, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya 1998 au Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1996. Sikiliza sehemu ya mchango wangu kwenye mjadala huo.


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-03-04T22_10_40-08_00.mp3
Mahojiano na Waziri Phillip Marmo Juu ya Wagombea Binafsi

Wed, 03 Mar 2010 06:31:19 +0000

(image)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo (pichani) amesema kuwa serikali haitokaidi uamuzi wa Mahakama kuhusu suala la wagombea binafsi endapo Mahakama ya Rufani itasisitiza kuwa waruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu ujao kama ilivyoamuriwa na Mahakama Kuu mwaka 2005. Hata hivyo, Bw. Marmo amesema kuwa kutokana na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu kufikia mbali endapo msimamo wa mahakama utakuwa ni ule ule basi itabidi uchaguzi mkuu uahirishwe ili kuruhusu utaratibu wa kubadili Katiba na kuwezesha wagombe huru na binafsi kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu. Pamoja na hilo Bw. Marmo amedokeza kuwa endapo itabidi Katiba ibadilishwe basi kuna uwezekano kuwa suala la mgombea binafsi litarudishwa kwa wananchi ili liamuliwe kwa kupitia kura za maoni. Akizungumza na KLHN International ambacho ni kituo cha Watanzania kirushacho matango kupitia mtandao wa Intaneti Bw. Marmo alisema kuwa hata hivyo kwa wakati huu suala la kura za maoni halipo “kwani tutavuka huo mto tukiufikia”. Kuhusu kile ambacho kinaonekana kuwa ni mgongano kati ya serikali na mahakama kuhusu suala la mgombea binafsi Bw. Marmo alisema kuwa hakuna mgongano wowote isipokuwa hivi sasa haupo muda wa kutekeleza uamuzi wa mahakama akidai kuwa rufaa iliyokatwa na serikali ilisababisha uamuzi wa awali usitekelezeke. Bw. Marmo alitumia mfano wa adhabu ya kifo ambapo rufaa ikikatwa basi adhabu ya awali ya kunyongwa haitekelezwi hadi rufaa iamuliwe. Hata hivyo alipoulizwa kwa kutumia mfano wa kesi ya Nalaila Kiula (aliyekuwa Waziri wa Ujenzi) na ile ya kina Nguza Viking ambapo wote licha ya kukata rufaa bado waliendelea kutumia adhabu zao Bw. Marmo alidai kuwa “kesi hizo ni za mazingira tofauti”.


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-03-02T22_31_19-08_00.mp3
Mahojiano ya Mwanakijiji na PowerBreakfast - Clouds FM

Thu, 14 Jan 2010 07:10:15 +0000

(image)
Nimepata nafasi ya kuzungumza kwa muda mrefu na mojawapo ya vipindi maarufu nchini Tanzania kile cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM. Nilizungumza na Bw. Gerald Hando. Hii ni sehemu ya mahojiano hayo.


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-01-13T23_10_15-08_00.mp3
Mahojiano na Chama cha Msalaba Mwekundu na Mpango wa kusaidia wahanga wa Mafuriko!

Sun, 10 Jan 2010 06:05:16 +0000

(image)
Unaweza kupata mpango tulio nao hadi hivi sasa wa kushiriki katika kuchangia wahanga wa mafuriko yanayoendelea nchini kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu. Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mkuu wa Kitengo cha Maafa wa chama hicho nchini Bw. Joseph Kimaryo ambaye anatueleza hali ilivyo hadi hivi sasa (Jumamosi Januari 9, 2010). Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea. Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM). Pata nakala ya mpango huo hapa: http://www.box.net/shared/g99no7hjkg


Media Files:
http://mwanakijiji.podOmatic.com/enclosure/2010-01-09T22_05_16-08_00.mp3